FRIED EGGPLANT 🍆


FRIED EGGPLANT / BILINGANYA ZA KUKAANGA:

Mahitaji :

Bilinganya 3 Kubwa
Mayai 5
Unga wa ngano Kikombe 1
Chumvi Kiasi Chako
Pilipili manga ya Unga 1/2 kjk cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kjk cha chai

Jinsi ya kupika :

Safisha na chuja maji kisha kata vipande vipande vya bilinganya na loweka ndani ya maji ya chumvi (5 vikombe maji + 2 vya chai chumvi) kwa kuzuia kugeuka rangi nyeusi.

Changanya pamoja mayai, unga, chumvi  na pilipili manga na ya unga pamoja.
Weka chombo jikoni na weka mafuta ya kutosha. Mafuta yakishapata moto, chovya bilinganya ndani ya mchanganyiko wa mayai na kuziweka katika mafuta ya moto (kipande kwa kipande) na kaanga mpaka viwe rangi ya dhahabu. Usikaange zikawa nyeusi sana zitakua chungu.

Baada ya kuipua kutoka katika karai ya mafuta weka juu ya kitambaa jikoni kwajili kunyonya mafuta ya ziada. Kisha weka katika sahani maalum. Na bilinganya tayari kuliwa.

Hakikisha usiweke vipande vingi mno kwa mara moja, vinginevyo bilinganya zitanyonya mafuta sana.
Pia, mafuta lazima  yawe ya moto wa kutosha si makali sana vinginevyo bilinganya zitanyonya mafuta sana

No comments:

Post a Comment