VIPIMO
Mchele wa pishori (basmati) 4
Nyama ya kuku bila mafupa 1 Lb
Kamba saizi kubwa 1Lb
Mchanganyiko wa mboga - njegere, karoti,
mahindi, maharage ya kijani (spring beans) 2 vikombe
Figili mwitu (Cellery) 2 mche
Vitunguu vya majani (spring onions) 4-5 miche
Kebeji 2 vikombe
Pilipili ya unga nyekundu 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Sosi ya soya 3 vijiko vya supu
Mafuta 1/4 kikombe
Chumvi kiasi
NAMNA YA KUPIKA NA KUTAYARISHA
1. Osha na roweka mchele.
2. Tia kamba chumvi na pilipili nyekundu ya unga. Tia mafuta vijiko viwili katika kikaango (frying pan), kaanga kamba kidogo tu, weka kando.
3. Katakata kuku vipande vidogo vidogo, tia chumvi na pilipili manga. Kaanga kaTika kikaango (ongeza mafuta kidogo) Weka kando.
4. Katika karai, tia mafuta kidogo kama vijiko vitatu vya supu, tia kamba na kuku, tia mboga za mchanganyiko, sosi ya soya na chumvi, kaanga kidogo. (Kama mboga sio za barafu) itabidi uchemshe kidogo.
5. Katakata kebeji, figili mwitu (cellery) na vitunguu vya majani (spring onions) utie katika mchaganyiko. acha kwa muda wa chini ya dakika moja katika moto.
6. Chemsha mchele, tia mafuta kidogo au siagi, chumvi upikie uive nusu kiini, mwaga maji uchuje.
7. Changanya vyote na wali rudisha katika sufuria au bakuli la oveni, funika na upike kwa moto wa kiasi kwa muda wa dakika 15-20 takriban.
8. Epua na upakue katika sahani ukiwa tayari kuliwa.
No comments:
Post a Comment