PILAU YA KUKU
Vipimo
Mchele 1 kilo
Kuku 1
Vitunguu 3
Viazi/mbatata 5
Jira/bizari ya pilau nzima 3 vijiko vya supu
Mdalasini 1 kijiti
Pilipili manga 1 kijiko cha supu
Hiliki 3 chembe
Karafuu 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia ½ kikombe
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote..
Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
Tia bizari zote isipokuwa hiliki.
Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo.
Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment