SIMPLE BUTTER CREAM FROSTING FOR CAKE 🎂


SIMPLE BUTTER CREAM FROSTING FOR CAKE / ICING SIMPLE YA KUPAMBIA CAKE :

Mahitaji :

1/2 kikombe siagi
1- 1/2 kjk cha Chai Vanilla essence
Vikombe 2 icing sugar iliochekechwa
Vjk 2 vya kulia maziwa
Rangi  ( hiari yako )

Maelezo :

Katika bakuli ya kiasi weka siagi kisha ipige na machine ya  cake ya mkono au mwiko mpaka siagi ivimbe na ibadilike rangi.
Miminia icing sugar na vanilla essence kisha piga tena. Weka maziwa na piga kwa dakika 3-4 zaidi.
Kama huweki rangi hapo ndio icing yako tayari. Na kama utaweka rangi basi weka rangi na upige tena na uangalie kiasi cha rangi utakayopenda ukoleaji wake.
Unapambia kama hapo katika picha. Ukipenda pakaza cake nzima

No comments:

Post a Comment