TAMBI ZA DENGU


TAMBI ZA DENGU

Mahitaji :

🔸Unga wa dengu kilo 1
🔸Chumvi kiasi
🔸Pilipili manga kiasi
🔸Pilipili ya unga kiasi
🔸Manjano kijiko 1 cha chai
🔸Baking soda 1/2 kijiko cha chai
🔸Mafuta ya kula  kikombe 1
🔸Maji vugu vugu kiasi cha kukandia

NAMNA YA KUTAYARISHA:

1. Changanya vitu vikavu vyote vizuri katika bakuli, tia mafuta kisha changanya tena ufanye chenga.

2. Anza kutia maji taratibu hadi upate unga mlaini, paka mikono yako mafuta kisha kanda unga kwa muda wa dk 5

3. Funika na uache ukae kwa muda muda wa dk 10. Bandika mafuta jikoni juu ya moto wa kiasi

4. Utie unga wako katika mashine ya tambi kisha binya taratibu kuruhusu tambi kutoka na kudondoka kama mvua katika mafuta ya moto kisha taratibu zungusha mzunguko mmoja na acha ziive na kupata rangi pande zote mbili (angalia picha katika comments)

5. Epua katika chujio zichuje mafuta, rudia utaratibu kwa unga wote. Taratibu zivunje vunje na tambi zako zitakuwa tayari kwa kula.

No comments:

Post a Comment