VANILLA TEA WITH SPICES
VANILLA CHAI WITH SPICES / CHAI YA VIUNGO YA VANILLA :
Mahitaji :
Maji vikombe 5
Pilipili manga 6
Karafuu 6
Kungu manga kjk 1 cha chai
Hiliki ya unga kjk 1 cha chai
Tangawizi ilopondwa 1/2 kjk cha chai
Mdalasini 3
Majani ya chai vifuko 6
Sukari vjk 4 vya kula
Vanilla kjk 1 cha chai
Maziwa vikombe 4
Maelekezo
Weka kwenye sufuria maji, pilipili manga, karafuu, hiliki, tangawizi, kungumanga na mdalasini.
Chemsha kwa dakika 5 au zaido kila ikichemka viungo vinazidi kutoa harufu nzuri
Zima moto na weka majani ya chai acha kwa dakika 5-6
Tia sukari na vanilla koroga
Pasha maziwa yakipata moto mimina kwenye mchanganyiko wa viungo na koroga
Andaa kuinywa...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment