PLUMS CAKE / CAKE YA MATUNDA DAMU

Mahitaji

60 grams siagi
112 g sukari
Ganda ya limao 1 lililokwanguliwa
2 mayai
170 g unga
1/2 kjk cha chai baking powder
¼ kikombe maziwa
5-6 matunda damu yaliyomenywa na kukatwakatwa
Sukari iliyosagwa kwajili ya kunyunyiza juu ya matunda damu.

Maelekezo:

Washa oven kwa moto 350˚f. Unaokea hata katika mkaa kama unavyopalilia Wali.
Chukua chombo cha cake na pakaa siagi na nyunyizia unga kwa mbali na weka pembeni.

Changanya siagi, sukari na ganda la ndimu lililokwanguliwa. Kisha weka yai moja piga vizuri kisha weka na yai la pili piga vizuri.

Weka nusu ya unga na baking powder  endelea kwa kuchanganya na kijiko cha mbao au mwiko. Mimina nusu ya maziwa na endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri.
Weka nusu ya unga uliobakia na changanya tena kisha mimina nusu ya maziwa yaliobakia na changanya tena vizuri.

Mimina mchanganyiko katika chombo cha kuokea cake. Weka vipande vya matunda damu juu ya cake. Kisha nyunyizia sukari iliyosagwa kidogo.
Oka kwa dakika 45 au mpaka kijiti kikiingizwa katika keki kitoke nje kisafi na rangi ya cake juu iwe dhahabu.
Acha cake ipoe. Baada ya hapo cake tayari kuliwa

No comments:

Post a Comment