SPHAGETTI BOLOGNESE

MAHITAJI:
1. Tambi mfuko mmoja
2. Nyama ya kusaga nusu kilo
3. Nyanya 4
4. Kitunguu swaumu 1
5. Kitunguu maji kikubwa 1
6. Njegere glass ndogo 1{optional} 
7. Karoti 1 na Hoho 1
8. Chumvi kiasi
JINSI YA KUANDAA:
-Weka mafuta yachemke,kisha kaanga kitunguu swaumu kilichopondwa pamoja na kitunguu maji,hoho na karoti.
-Weka nyama, yama katika mchanganyo huo na ikaange hadi itakapobadilika rangi kuwa ya brown.
-Weka tambi zilizochemshwa na njegere.
-Koroga kisha ongeza nyanya(ni vizuri zikawa zimesagwa kuliko kukatwakatwa) kisha ongeza maji kidogo.
-Funika acha ichemke,kisha weka chumvi.
-tayar kwa kuliwa, inaweza kuliwa kama chakula cha wakati wowote,pamoja na kinywaji chochote. Enjoy

No comments:

Post a Comment