MAKANGE YA NYAMA
*MAKANGE YA NYAMA YA NG'OMBE*
*MAHITAJI*
Nyama steak nusu kilo
Hoho 1
Karoti 1
Nyanya 1 au tomato ketchup (sio lazima )
Kitunguu maji kikubwa 1
Limao 1
Saum ya unga
Tangawizi
Beef masala
Pilipili manga
Mafuta na chumvi
*KUANDAA NA KUPIKA*
💐Katakata nyama yako kwa umbo last urefu
💐Osha nyama yako kisha iweke viungo saum , Pilipili manga na Tangawizi na chumvi na limao nusu
💐Kisha changanya vizuri weka pembeni viungo vikolee
💐Katakata hoho na Karoti kwa staili ya urefu kama ulivyokata nyama na vitunguu kata staili upendayo kisha vichambue kimoja kimoja
💐Saga nyanya kwa blenda au kwangua
*KUPIKA*
💛Weka sufuria jikoni kisha tia Mafuta yakipata moto weka nyama anzaa kukaanga ikiisha ubichi weka kitunguu acha iendelee kujipika ukiona maji yanaishi weka nyanya au tomato ketchup (sio lazima) geuza ili ienee kwenye nyama kisha weka hoho na caroti ongeza chumvi kiasi chako pika kwa dk 5 na makange yatakuwa tayari.
_UNAWEZA KULA KWA UGALI VIAZI CHAPATI WALI AU CHOCHOTE UPENDACHO
Maelezo ya picha kwenye comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment