MILK CAKE

MILK CAKE / KEKI YA MAZIWA

VIPIMO

Siagi -  Kikombe 1
Sukari -  Kikombe 1
Unga - Vikombe 2
Maziwa - Kikombe ½
Mayai -  4
Baking Powder - Kijiko cha supu 1
Arki rose -  kidogo

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Washa oveni 350 - 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.

2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.

3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.

4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.

5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)

6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.

7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.

8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.

Enjoy!

No comments:

Post a Comment