MAHAMRI

MAANDAZI / MAHAMRI

VIPIMO

Unga - vikombe vya chai 4
Sukari - kikombe cha chai 1
Hamira - kijiko cha chai 1
Samli - kijiko cha chai 1
Maziwa au Tui la nazi - kikombe cha chai 1½
Hiliki -  kiasi
Mafuta ya kukaangia -  kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Changanya unga  Hamira, Samli, maziwa au tui, kisha vuruga na kanda ukandike kiasi.
 
2. Kata madonge manane kisha acha uumuke.    

3. Ukishaumuka sukuma kila donge ukate vipande vinne.

4. Panga kwenye meza tena yaumuke. Weka mafuta ya kukaangia katika karaii na yakaange kwa moto wa kiasi.

5. Yatoe weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.  

Enjoy!

No comments:

Post a Comment