MANGO JAM

MANGO JAM / JAM YA EMBE :

Mahitaji :

Maembe 4 yalowiva
Sukari 3/4 kikombe
Maji ya limao au ndimu 1 kubwa

Maelekezo  :

1. Menya maembe na katakata vipande tupa makokwa. Weka vipande vya maembe, sukari na maji ya limao kwenye sufuria, injika jikoni moto wa kati ichemke
2. Sukari ikiyayuka na ikianza kufanya mapovu punguza moto na weka moto mdogo
3. Acha kiasi cha dakika 5-6 maembe yapate kuwiva, na unaweza kuyaponda ponda wakati ikiendelea kuwiva
4. Wakati inawiva utaona maembe yamepondeka na imekuwa nzito endelea kuipika kwa dakika 3
5. Ijaribu jam kama iko tayari, chota jam kwa kutumia mwiko na uchore mstari kwenye sahani. Mstari ulouchora uwe umegandia na sio wenye kuchuruzika. Jam itakuwa tayari
6. Zima jiko na acha jam ipoe, kila inapokaa itazidi kuwa nzito
7.  Andaa kopo la kuhifadhia  jam na ikipoa hamishia kwenye kontena na ihifadhi kwenye friji kiasi cha siku 10 -12 au hadi itakapoisha
8. Furahia kula mkate ulopakwa jam ilotengenezwa nyambani.


No comments:

Post a Comment