CAPSICUM RICE / PILAU YA HOHO
viungo:
Saga pamoja katika blender :
vitunguu swaumu - 5
tangawizi - ndogo kipande
Pipili za kijani - 2
nyanya - 3
Weka pembeni.
Viungo kwajili ya Pilau :
mafuta - kiasi chako
Kijiti cha mdalasini - ndogo kipande
karafuu - 2
kitunguu maji - 1/2 kikombe - vilivyokatwa
viazi ulaya - 1 kikombe vilivyokatwa
Hoho za kijani - 2 vikombe -zilizokatwa
basmati mchele au mchele wa kawaida 1 kg
garam masala - 1/2 kjk cha chai
manjano - kidogo
Pilipili ya unga - 1/2 tsp (sio lazima)
chumvi - kwa ladha
Majani ya giligilani 1 kikombe yaliyokatwakatwa.
Maelezo:
Weka sufuria jikoni na weka mafuta na kisha weka karafuu, mdalasini, kitunguu maji na vile viungo ulivyosaga katika blender na pika mpaka vitunguu viive.
Kisha weka viazi, hoho na mchele, garam masala, manjano,pilipili ya unga na chumvi.
Pika na kupalilia pilau ya hoho kama kawaida.
Wali ukishaiva baada ya kupakua mwagia majani ya giligilani na pilau ya hoho tayari kuliwa na mchuzi au mboga yeyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment