GRILLED RIBS/ NYAMA YA MBAVU ZA NG'OMBE YA KUCHOMA :
Mahitaji :
Nyama ya mbavu kilo 1
Kitunguu swaumu kjk 1 cha kulia
Tangawizi kjk 1 cha kulia
Soy sauce 1/2 kikombe au zaidi
Pilipili mbichi 3 zilizotwangwa
Kjk 1 cha chai binzari nyembamba ya unga
Asali 1/2 kikombe cha chai
Ndimu kiasi chako
Majani ya giligilani 1/2 fungu yaliyokatwa
Maelezo :
Osha nyama na iwe safi na katakata. Kisha weka kwenye chungio muda wa dikika 10 ichuje maji.
Baada ya dikika 10 weka katika chombo kingine na mahitaji yote yaliyosalia isipokua majani ya giligilani.
Roweka nyama siku nzima au usiku kucha kwenye fridge baada ya hapo tayari kuchoma katika mkaa. Wakati unachoma nyama mwagia sauce juu ya nyama ili izidi kukolea viungo. Ikishaiva tayari kwa kula weka kwenye sahani na pambia kwa kumwagia majani ya giligilani na kula na chip's au mkate au ndizi za kuchoma.
No comments:
Post a Comment