FRIED EGGPLANT / BILINGANYA ZA KUKAANGA :
Mahitaji :
Bilinganya 2 zilizokatwa kwa urefu
Pilipili mbichi nyekundu 2 zilizotwangwa
Siki kiasi ( vinegar nyeupe )
Majani ya giligilani 1/2 fungu
Maelezo :
Roweka vipande vya bilinganya kwa kuchanganya mahitaji yote isipokua majani ya giligilani. Na acha ikae lisaa limoja.
Baada ya hapo kaanga katika karai la mafuta ya kutosha. Hakikisha zinaiva vizuri. Chuja mafuta na weka katika sahani mwagia majani ya giligilani na tayari kula na wali.
No comments:
Post a Comment