KATLESI ZA NYAMA

KATLESI ZA NYAMA

VIPIMO NA NAMNA YA KUTAYARISHA

Mbatata / viazi Chemsha - ½
Nyama ya kusaga kilo 1
Mayai Piga kwa uma (fork katika kibakuli) - 3
Vitunguu maji katakata vidogodogo (chopped) - Vikubwa 2
Pilipili shamba/mbichi ilosagwa - kijiko cha chai 1
Ndimu / limau Kamua - au mbili 1
Pilipili manga - kijiko cha chai ½
Tangawizi mbichi Saga - kipande 1
Kitunguu thomu Saga - chembe 7 – 1
Uzile (cumin) Saga - kijiko vya chai 1
Bizari ya mchuzi ukipenda - kijiko cha chai 1
Kotmiri majani osha, katakata (chop) - 1 kikombe 1
Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani ya chali - kikombe 1
Mafuta

NAMNA YA KUPIKA

1. Menya mbatata / viazi.

2. Chemsha Nyama kwa tangawizi na kitunguu thomu, ndimu, au limau mpaka akauke.

3. Ziponde mbatata katika bakuli mpaka zivurugike.

4. Changanya vizrui na mbatata / viazi, nyama na viungo vyote vinginevyo isipokuwa chenga za mkate na mafuta, na mayai.

5. Fanya madonge uviringe kama shepu ya yai.

6. Chomva katlesi ndani ya mayai halafu karagiza kwenye bread crumbs.

7. Weka mafuta yashike moto, zitie katelsi mpaka zigeuke rangi ya dhahabu zitowe tayari kwa  kuliwa.

Enjoy!


No comments:

Post a Comment