MEAT STUFED DINNER ROLLS / BUNS ZA NYAMA:

MEAT STUFED DINNER ROLLS / BUNS ZA NYAMA:

Mahitaji :

Kwajili ya Buns :
Vijiko 1-1 / 2 hamira
1/2 kikombe maji ya vuguvugu
Vijiko 3 vya kulia sukari
1 yai kubwa
1/2 kijiko cha chai chumvi
2-1 / 4 vikombe unga

Kwajili ya Nyama :
Kilo 1 ya nyama ya kusaga au kuchambuliwa
Vikombe 1-1 / 2 cabbage iliokatwa
1/2 kikombe cha kitunguu maji kilichokatwa
Chumvi na pilipili manga kiasi chako
1/2 kikombe jibini ( sio lazima )
Vijiko viwili vya siagi, ilioyeyushwa

Maelekezo :

Katika bakuli kubwa, yeyusha hamira kisha weka sukari, yai, chumvi na unga 1 kikombe; kanda polepole kwa dakika 3. Ongeza unga wa kutosha uliobaki ili upate donge laini. Endelea kukanda mpaka  donge liwe laini na kuvutika kwa kiasi cha dakika 6-8.
Chukua bakuli lingine pakaza mafuta na weka donge na kisha paka mafuta kidogo juu ya donge. Funika na acha mahali pa joto hadi donge liumuke, takriban lisaa 1.

Katika chombo kikubwa, weka nyama na pika kwa moto wa kati mpaka iive vizuri. Ongeza kabichi, vitunguu, chumvi na pilipili. Funika na pika kwa moto mdogo mpaka nyama na cabbage viive kwa muda wa dakika 15.
Weka jibini kama unayo kama huna epua kutoka jikoni na weka kando ili ipoe.

Chukua donge la scones na ugawanye vipande 12. Tengeneza donge la kutosha kuweka nyama ndani yake na kulibana vizuri. Kisha panga madonge katika chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta.
Acha na funika kwa muda wa nusu saa ili madonge yaumuke tena. Pakaza kwa brush siagi juu ya madonge. Oka kwenye oven kwa moto wa 350° kwa dakika 20 na kama unaoka kwenye mkaa basi hakikisha zinakua rangi nzuri ya dhahabu na buns za nyama tayari kuliwa.

No comments:

Post a Comment