BEEF ROAST

BEEF ROAST
Mahitaji :

Nyama ya Ng'ombe ya kawaida kilo 1 iliyochemshwa na kuiva.
Vitunguu maji vilivyokatwakatwa 2
Kitunguu swaumu 1/2 kjk cha chai
Tangawizi 1/2 kjk cha chai
Nyanya zilizokatwakatwa 15
Viazi mviringo vilivyokaangwa 10
Curry powder kjk 1 cha chai
Garam masala kjk 1 cha chai
Mdalasini wa unga kjk 1 cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kjk cha chai
Chumvi kiasi chako
Mafuta ya kupikia kiasi
Majani ya giligilani 1/2 fungu

Maelezo :

Bandika chombo na weka mafuta.. yakipata moto weka Vitunguu maji kaanga mpaka vikikaribia kufikia kua rangi ya dhahabu weka tangawizi na kitunguu swaumu na curry powder,garam masala,mdalasini wa unga,pilipili ya unga.
Kaanga kwa dakika 1. Kisha weka nyanya na nyama na Viazi na chumvi...kaanga mpaka nyanya zilainike kidogo. Wakati unakaanga kama roast linakaukia utaweka supu kidogo kidogo.
Endelea kukaanga mpaka nyanya zinalainika kabisa na mafuta yanajitokeza.
Inategemea na uzito wa roast unaotaka.
Mwagia majani ya giligilani kwa juu.

Baada ya hapo roast tayari kuliwa na chapati.

KATLES ZA SAMAKI


Mahitaji:

viazi kiasi 1/2 kilo
Samaki 1
mdalasini wa unga kijiko cha chai 1
Binzari nyembamba kijiko 1 itwange
Majani ya Kotmir fungu 1
Kitunguu swaum kilichopondwa kijiko 1 cha chai
Kitunguu maji 1 katakata
Ndimu 1
Chumvi kiasi
Pilipili manga 1/2 cha chai
Binzari manjano kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kupikia kiasi
Chenga za mkate kiasi
Mayai 2 yaliyopigw kabisa

JINSI YA KUPIKA  :

1.Chemsha samaki mtie,swaum mdalasini,binzari nyemba,chumvi,manjano ,pilipili manga na ndimu na maji kidogo kama robo kikombe tu.mchemshe akaukie kisha mtoe miba yote halafu mvuruge achanganyike vizuri na viungo

2.Chemsha viazi na maji kiasi  ,vitie chumvi,vitunguu maji na kotmir na thoum kidogo vikiiva tu vichuje maji kisha viponde ponde vizuri kisha tia ule mchanganyiko wa samaki halafu tengeneza shepu ya katlesi upendayo

3.Chovya katika chenga za mkate kisha chovya katika yai kisha kaanga katika mafuta lkn mafuta yawe kidogo yasifunike katles, kaanga zikiwa brown toa zichuje mafuta.katles tayari kuliwa na chatne yoyote upendayo

SIMPLE CAKE :

SIMPLE CAKE :

Siagi kikombe 1
Sukari kikombe 1
Mayai 4
Baking powder kijiko cha chai 1
Unga wa ngano kikombe 1 na nusu
Vanilla kijiko 1 cha chai

JINSI YA KUANDAA.

1.Kwenye bakuli tia Unga wa ngano na baking powder changanya vizuri kwa kijiko weka pembeni

2.Washa oven  180c kama unapikia mkaa koleza jiko kabisa.

3.Saga siagi na sukari mpaka iwe laini, tia yai moja moja huku uwe unasaga vizuri mpaka mayai yamalizike  , tia vanila changanya tena vizuri,

4.Tia unga wa ngano , saga  kidogo tu malizia kukoroga na mwiko.
Paka mafuta kwenye trey chini ili cake isigande , tia mchanganyiko wako ueneze vizuri na ubake mpaka iwive, ichome na kijiti, kujiti kikitoka  kikavu cake imewiva itoe, iwache ipoe kwa dakika 10 mpaka 15.
Kama unapikia kwenye mkaa weka moto juu na chini kama moto wa kupalilia wali.

5.Ikate kate vipande saiz unayotaka,kula na juice,chai n.k ENJOY. IMETUMIKA MEASURING CUP KWAJILI YA KUPIMIA VIPIMO NA HAIJATIWA MAZIWA!

FISH FINGER :SAMAKI


      FISH FINGER (SAMAKI)

MAHITAJI :A:
💎Unga wa ngano vijiko vikubwa 3
💎Kitunguu thoum kijiko 1
💎Binzari manjano kijiko 1
💎Curry powder kijiko
 1
💎Pilipili manga 1/2 kijiko
💎Pilipili ya unga kijiko1
💎Chumvi kiasi chako
💎Tangawizi iliyopondwa kijiko 1
💎mayai 2

MAHITAJI :B:

💎Samaki (mnofu) vipande 3 vikubwa,katakata vipande virefu virefu kama katika picha inavyoonesha.
💎Mafuta ya kukaangia kiasi
💎Chenga za mkate

JINSI YA KUPIKA
1.Changanya mahitaji  :A: yote mayai yawe ya mwisho kisha, changanya vizuri.

2.Tia vipande vyako vya samaki, halafu wachanganye vizuri waenee viungo kisha
acha kwa dakika 30

3.Chovya kipande kimoja kimoja katika chenga za mkate kisha tia ktk mafuta yaliyokwisha pata moto vizuri,kaanga wakiwa rangi ya brown watoe wachuje mafuta,tayari kwa kula na wali,ugali,chipsi ,chapati n.k.ENJOY!!!

NB;Samaki mwenye mnofu mweupe hupendeza zaidi lakini ukikosa tumia yoyote.

Karibuni....